2 Chronicles 36:5-8

Yehoyakimu Mfalme Wa Yuda

(2 Wafalme 23:35–24:7)

5 aYehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na mmoja. Akafanya maovu machoni pa Bwana Mungu wake. 6 bNebukadneza mfalme wa Babeli akamshambulia na kumfunga kwa pingu za shaba akampeleka Babeli. 7 cNebukadneza akachukua pia vyombo kutoka Hekalu la Bwana na kuviweka katika hekalu lake
Au: katika jumba lake la kifalme.
huko Babeli.

8 eMatukio mengine ya utawala wa Yehoyakimu, machukizo aliyoyafanya na yote yaliyoonekana dhidi yake, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda. Naye Yehoyakini mwanawe akawa mfalme baada yake.

Copyright information for SwhNEN